Ruka hadi maudhui
Moduli kumi na mbili

Kila kitu shule inachohitaji, kwenye mfumo mmoja

Moduli kumi na mbili zilizojengwa kuzunguka maisha ya kila siku ya shule za Tanzania. Bofya moduli yoyote upate mwongozo wake hatua kwa hatua.

Wanafunzi

Sajili kwa fomu au Excel, madarasa na mikondo, wasifu, picha, waliofukuzwa na wahitimu. Namba za usajili wazazi wanazotumia kuingia.

Soma mwongozo

Uchakataji wa matokeo

Walimu wanapakia alama za somo lao; mfumo unahesabu CA + mtihani, wastani, gredi, divisheni/pointi, nafasi na kuchapisha ripoti zenye nembo yako.

Soma mwongozo

Ada na uhasibu

Muundo wa ada kwa darasa, malipo yenye risiti, salio na madeni, mapato na matumizi, bajeti, trial balance na taarifa ya mapato.

Soma mwongozo

Wazazi wanalipa kwa simu

Lipa Ada: USSD push, namba ya malipo kwenye M-Pesa / Airtel / Mixx / Halopesa / CRDB, au benki na kadi. Inaingia yenyewe kwenye vitabu vya shule na risiti.

Soma mwongozo

SMS na WhatsApp bure

Matokeo, madeni, matangazo na risiti kwa wazazi kwa WhatsApp bure (SMS ikishindikana). Ripoti za usambazaji na gharama.

Soma mwongozo

Sehemu ya wazazi

Mzazi anaingia kwa namba ya mwanafunzi: matokeo, maoni, mahudhurio, malipo, kilichofundishwa, habari za shule.

Soma mwongozo

Tathmini na mahudhurio

Maoni ya mwalimu wa darasa kila muhula; mahudhurio ya siku na mwezi yenye ripoti na ujumbe wa waliokosekana.

Soma mwongozo

Ratiba

Mfumo wa vipindi, ratiba ya kiotomatiki bila kugongana, ratiba za walimu na ripoti za vipindi.

Soma mwongozo

Ufuatiliaji wa silabasi

Pakia mada; baada ya kila kipindi mwalimu anathibitisha alichofundisha kwa WhatsApp; dashibodi inaonyesha coverage ya kila darasa.

Soma mwongozo

Walimu na HR

Wafanyakazi, nafasi, walimu wa madarasa na masomo, likizo, mishahara na PAYE, rejista ya mali, app ya walimu.

Soma mwongozo

E-learning na mitihani

Vifaa vya kujifunzia, kazi na mitihani ya mtandaoni yenye maswali yanayosahihishwa yenyewe.

Soma mwongozo

Matukio na mashindano

Endesha tamasha za kitaaluma na vipaji, usajili, timu, ligi, picha.

Soma mwongozo
Kwa nini FAMNET

Kwa nini shule zinahamia FAMNET

Wazazi wanapokea ujumbe kweli

WhatsApp kwanza, SMS pale tu inapohitajika. Matokeo, risiti na vikumbusho vya madeni vinawafikia wazazi bila gharama ya SMS — hadi 500 kwa siku kwa shule, bure.

Ada zinakusanywa haraka

Wazazi wanalipa wakiwa nyumbani kwa mobile money au benki; mhasibu anapata uingizaji na risiti yenyewe. Madeni yanapungua, foleni zinatoweka.

Lugha mbili tangu msingi

Wazazi wanaona Kiswahili; walimu wanafanya kazi kwa Kiingereza; Kituo cha Msaada kinajibu kwa zote mbili.

Hakuna cha kusakinisha

Inafanya kazi kwenye kivinjari chochote, simu au kompyuta; nakala rudufu kila siku; data ni yako na inaweza kutolewa kwa Excel wakati wowote.

Nafasi na ukaguzi

Ngazi za matumizi zinaamua nani anasajili wanafunzi, nani anaingiza fedha na nani anachapisha matokeo; malipo yaliyohaririwa yanarekodiwa.

Msaada wa kweli

Msaada kwa WhatsApp, Kituo cha Msaada chenye miongozo 60+, na msaada wa kuanza kwa shule mpya.

Ione kwa data zako mwenyewe

Sajili, pakia darasa moja kwa Excel ukachapishe ripoti leo.