Ruka hadi maudhui

Siwezi kuingia / natolewa nje mara moja

Sababu za kawaida: mtindo wa jina la mtumiaji si sahihi, akaunti haijathibitishwa au inakaguliwa, cookies zimezuiwa, au huduma imesitishwa.

Imesasishwa 06/10/2026
  • “Invalid username or password” — walimu watumie simu kama 0XXXXXXXXX; wazazi namba ya usajili + jina la mwanafunzi; wasimamizi namba ya usajili au barua pepe. Manenosiri yanajali herufi kubwa/ndogo.
  • “Your account is not yet verified” — fungua kiungo/msimbo wa uthibitisho uliotumwa kwa barua pepe ya shule, au omba msaada wathibitishe.
  • “Your account is under review” — usajili unakaguliwa; wasiliana na [email protected].
  • Unarudishwa moja kwa moja kwenye ukurasa wa kuingia — cookies zimezuiwa (private mode, kivinjari cha ndani ya app). Fungua tovuti kwa Chrome/Safari, ruhusu cookies, au futa data ya tovuti ujaribu tena.
  • “Service Suspended — System Fee Not Paid” — soma ada ya mfumo.
  • Mwalimu anaona menyu tupu — bado hajapangiwa nafasi/madarasa/masomo: mpangie.

Hukupata jibu? Andika WhatsApp kwa msaada wa FAMNET: 0722 279 412 (ujumbe tu), piga simu 0753 464 603 (simu tu), au barua pepe [email protected].