Ruka hadi maudhui

Kuingiza malipo ya mwanafunzi na kuchapisha risiti

Mhasibu anarekodi kila slip ya benki au malipo ya cash kwa mwanafunzi na aina ya ada; mfumo unatoa namba ya risiti na kusasisha salio.

Imesasishwa 06/10/2026

Payments › Enter Payments (O-Level / A-Level / Students Payments). Ukurasa unaonyesha kwanza aina za ada na jumla zinazotakiwa kwa mwaka; bofya Click here to enter students payments for this academic year.

  1. Tafuta mwanafunzi (jina au namba ya usajili) ukafungue fomu ya malipo.
  2. Jaza: Payment type, Amount, Bank / account (kutoka Bank Accounts), Payment method (Bank deposit, Cash, Mobile money, Cheque), namba ya risiti/slip ya benki, Date deposited, mwezi.
  3. Submit. Mfumo unatengeneza batch na namba ya risiti ya shule (mf. R28265-26-534) na kuonyesha risiti ya Print; risiti ya WhatsApp/SMS inamwendea mzazi kama ujumbe umewashwa.

Aina kadhaa za ada zilizolipwa kwa slip moja zinaweza kuingizwa kwenye batch moja. Makosa: fungua malipo kutoka View Payments by list ukabofye Edit au Delete; marekebisho yanarekodiwa kwenye View Edited Payments.

Malipo yaliyofanywa na wazazi mtandaoni yanaonekana hapa yenyewe yakiwa na benki ClickPesa (Mobile Money) na issuer PARENT-ONLINE — usiyaingize tena.

Hukupata jibu? Andika WhatsApp kwa msaada wa FAMNET: 0722 279 412 (ujumbe tu), piga simu 0753 464 603 (simu tu), au barua pepe [email protected].