Ruka hadi maudhui

Orodha ya mipangilio ya shule mpya (fanya kwa mpangilio huu)

Mipangilio kumi inayotakiwa kuwepo kabla matokeo, ripoti na ada hazijafanya kazi — na njia ya menyu ya kila moja.

Imesasishwa 06/10/2026

Fungua Home › Go to Settings (Admin Settings). Ukurasa wa mwanzo unaonyesha Setup Overview yenye kadi za maendeleo. Kamilisha hizi kwa mpangilio:

  1. General Settings — taarifa za shule, nembo na School Header (inachapishwa kwenye kila ripoti). Maelezo
  2. Students / Class Settings — aina ya shule (O-Level / A-Level / zote; Primary / Nursery), aina ya wanafunzi (Day / Boarding / wote), mikondo ya madarasa (A, B, C…) na majina ya madarasa. Maelezo
  3. Subjects Registration — sajili masomo yote, kisha uyapangie kila ngazi ya darasa (tumia Bulk Assign). A-Level: sajili Combinations. Maelezo
  4. Mode of Assessments — asilimia ya CA na ya mtihani kwa kila ngazi. Maelezo
  5. Grades, Divisions, Points — mipaka ya gredi (A 75–100…), sheria za divisheni na pointi. Maelezo
  6. Results Calculation — Average au Division, na masomo yanayohesabika. Maelezo
  7. Evaluation — vigezo vya tathmini na gredi za maoni zinazotumiwa na walimu wa madarasa. Maelezo
  8. Payment Types → Fee Amounts → Installments → Priorities → Bank Accounts. Maelezo
  9. Access levels — nani anaruhusiwa kusajili wanafunzi, kuingiza malipo, n.k. Maelezo
  10. Go to system → sajili walimu, panga walimu wa madarasa na wa masomo, sajili wanafunzi. Kisha walimu wataweza kupakia matokeo.
Kila kitu kinaweza kuhaririwa baadaye, ila badilisha gredi/sheria za tathmini kabla ya kupakia alama za muhula — la sivyo utahesabu upya matokeo baadaye (Results › View Results › Recalculate).

Hukupata jibu? Andika WhatsApp kwa msaada wa FAMNET: 0722 279 412 (ujumbe tu), piga simu 0753 464 603 (simu tu), au barua pepe [email protected].