Ruka hadi maudhui

Kuingia — msimamizi wa shule, walimu na wazazi

Ukurasa mmoja wa kuingia, aina tatu za watumiaji. Kila mmoja anatumia jina na nenosiri gani.

Imesasishwa 06/10/2026

Kila mtu anaingia kupitia schools.famnet.co.tz → Login. Mfumo unatambua aina ya akaunti kutokana na jina la mtumiaji:

MtumiajiJina la mtumiajiNenosiriAnafika wapi
Msimamizi wa shule (akaunti ya mmiliki)School Reg Number (mf. S1234) au barua pepe ya shuleNenosiri ulilochagua wakati wa usajiliHome → Go to system / Admin Settings
Mwalimu / mfanyakaziNamba ya simu iliyoandikwa wakati wa kumsajili, kwa mtindo wa 0XXXXXXXXX (tarakimu 10)default mara ya kwanza — ibadilishe mara moja (Human Resource › Edit my info)Dashibodi ya mwalimu yenye menyu za nafasi yake tu
MzaziNamba ya usajili ya mwanafunzi (mf. OS121.2025.015)Jina kamili la mwanafunzi kama lilivyosajiliwa (au sehemu yake)Sehemu ya wazazi: wasifu, matokeo, malipo, Lipa Ada

Tiki Remember me kwenye kifaa chako binafsi ili usiingie kila mara.

Ukirudishwa kwenye ukurasa wa kuingia mara tu baada ya kuingia, kivinjari chako kinazuia cookies au umefungua tovuti kupitia kivinjari cha ndani ya app (mf. ndani ya Facebook). Fungua kwa Chrome/Safari ukaruhusu cookies.

Umesahau nenosiri? Soma Nenosiri lililosahaulika.

Hukupata jibu? Andika WhatsApp kwa msaada wa FAMNET: 0722 279 412 (ujumbe tu), piga simu 0753 464 603 (simu tu), au barua pepe [email protected].