Taarifa za matokeo, risiti za ada, vikumbusho vya madeni na matangazo sasa yanawafikia wazazi kwa WhatsApp kwanza. Ujumbe hauna kikomo cha herufi na hauigharimu shule chochote — hadi 500 kwa siku kwa shule kutoka namba ya pamoja ya FAMNET. Namba ya mzazi ikiwa haina WhatsApp, ujumbe ule ule unaenda kwa SMS kutoka salio la shule.
Shule zinazotaka wazazi waone namba yao zinaweza kujiunga (TZS 10,000/mwezi, ujumbe 2,000/siku) na kuunganisha simu ya shule kwa kuscan QR kwenye Admin Settings. Jinsi ya kuiweka.