FAMNET Schools (schools.famnet.co.tz) ni mfumo wa mtandaoni kwa shule za msingi, sekondari (O-Level na A-Level) na vyuo nchini Tanzania. Kila kazi ya shule ya kila siku inapatikana kwenye akaunti moja:
- Wanafunzi — usajili, madarasa na mikondo, wasifu, waliofukuzwa na wahitimu.
- Walimu na wafanyakazi — usajili, nafasi, walimu wa madarasa na masomo, HR na mishahara.
- Matokeo — walimu wanapakia alama za somo lao; mfumo unahesabu wastani, gredi, divisheni/pointi, nafasi na kuchapisha ripoti zenye kichwa na nembo ya shule yako.
- Tathmini na mahudhurio — maoni ya mwalimu wa darasa, mahudhurio ya kila siku/kila mwezi na ripoti zake.
- Ada na uhasibu — muundo wa ada kwa kila darasa, malipo yenye risiti, madeni, malipo yaliyoahirishwa, wazazi kulipa ada mtandaoni, mapato/matumizi na taarifa za fedha.
- Ujumbe — SMS na WhatsApp (bure) kwa wazazi na walimu: matokeo, madeni, matangazo.
- Ratiba na ufundishaji — vipindi, ratiba ya kiotomatiki, ripoti za vipindi, ufuatiliaji wa silabasi.
- E-learning na matukio — vifaa vya kujifunzia, kazi, mitihani ya mtandaoni, matukio ya shule.
- Sehemu ya wazazi — mzazi anaingia kwa namba ya usajili ya mwanafunzi akaona matokeo na malipo, akalipa ada moja kwa moja kutoka kwenye simu yake.
Mfumo una milango mitatu: Go to system (kazi za kila siku), Admin Settings (jinsi shule yako ilivyopangwa) na Sehemu ya wazazi.
Tumia kisanduku cha kutafuta juu ya ukurasa huu — andika neno kama matokeo, ada au ratiba.