Ruka hadi maudhui

Kuona matokeo, kuhesabu upya na kuchapisha ripoti

Students Results, Class Results na Consolidated Results: kila moja inaonyesha nini, jinsi ya kuhesabu upya baada ya marekebisho, na jinsi ya kuchapisha ripoti.

Imesasishwa 06/10/2026
  • Results › Students Results — chagua darasa, muhula na (ukipenda) miezi maalum → Search. Unapata orodha ya darasa na alama za kila mwanafunzi kwa kila somo, wastani/pointi, gredi, divisheni na nafasi. Fungua mwanafunzi upate ripoti kamili (yenye nembo, kichwa, maoni ya tathmini, mahudhurio na maelekezo ya ripoti) ukabofye Print; au chapisha ripoti zote za darasa kwa pamoja.
  • Results › View Class Results (walimu wa madarasa) — vivyo hivyo kwa madarasa uliyopangiwa.
  • Results › Consolidated Results — karatasi moja kwa kila darasa yenye masomo yote, jumla, nafasi na muhtasari wa gredi/divisheni; hutumika kwenye vikao vya walimu na mbao za matangazo.

Recalculate

Nafasi na wastani huhifadhiwa (cache). Baada ya kupakia tena alama, kubadilisha mipaka ya gredi, kuongeza mwanafunzi au kurekebisha masomo-ndani, bofya Recalculate kwenye ukurasa wa matokeo wa darasa/muhula huo.

Chapisha (Publish) kabla ya kuchapa ripoti: inawazuia walimu kubadilisha alama baada ya ripoti kutolewa na inafungua matokeo kwa wazazi.

Hukupata jibu? Andika WhatsApp kwa msaada wa FAMNET: 0722 279 412 (ujumbe tu), piga simu 0753 464 603 (simu tu), au barua pepe [email protected].