Ruka hadi maudhui

Aina za watumiaji na kila mmoja anaweza kufanya nini

Msimamizi wa shule, nafasi za wafanyakazi (Head, Academic, Finance, Teacher…), wazazi, na jinsi Access Levels zinavyoamua nani anafanya nini.

Imesasishwa 06/10/2026

Msimamizi wa shule

Akaunti iliyotengenezwa wakati wa usajili. Inaona kila kitu: Go to system na Admin Settings, na ndiyo pekee inayobadilisha mipangilio, kununua SMS au kulipa ada ya mfumo.

Nafasi za wafanyakazi

Kila mfanyakazi anasajiliwa na Title/Work (Teacher, Accountant, Secretary, Manager…), na walimu wanapewa pia Position kupitia Staffs › Teachers List › Change Position: Head, Second Head, Academic, Assistant Academic, Librarian, Lab Technician, Discipline, Dean au Normal Teacher. Menyu anazoziona mfanyakazi zinategemea nafasi hii:

  • Normal Teacher — Upload Results za masomo aliyopangiwa, Evaluate / Attendance / Report instructions za madarasa aliyopangiwa, ratiba, e-learning.
  • Academic / Head / Second Head — pamoja na kuchapisha matokeo, matokeo ya pamoja, ukamilifu wa alama, madarasa yote.
  • Finance / Accountant / Bursar — malipo, risiti, madeni, malipo ya ada mtandaoni, mapato na matumizi, ripoti za uhasibu.
  • Secretary / wengine — kadiri Access Levels zinavyowapangia.

Access Levels (shughuli → akaunti)

Admin Settings › Access levels: tiki shughuli (mf. Students registration) ukachague akaunti ya jumla (mf. Secretary). Kuanzia hapo kila mtumiaji aliye chini ya akaunti hiyo anafanya shughuli hiyo. Hivi ndivyo unavyomruhusu katibu kusajili wanafunzi au mhasibu kuingiza malipo bila kumpa nenosiri la msimamizi.

Wazazi

Wanaona tu: wasifu wa mwanao, matokeo (baada ya kuchapishwa), malipo na ukurasa wa Lipa Ada.

Hukupata jibu? Andika WhatsApp kwa msaada wa FAMNET: 0722 279 412 (ujumbe tu), piga simu 0753 464 603 (simu tu), au barua pepe [email protected].