Ruka hadi maudhui

Ada ya mfumo na mchango wa wazazi

FAMNET inalipiwaje: ama shule inalipa ada ya mfumo ya muhula/mwaka, ama kila mzazi analipa mchango wa mwaka (TZS 3,500 kwa mwanafunzi) anapoangalia matokeo.

Imesasishwa 06/10/2026

Njia A — wazazi wanalipa mchango (ya kawaida)

Mzazi wa kila mwanafunzi analipa mchango wa mfumo wa TZS 3,500 kwa mwaka mara ya kwanza anapofungua matokeo kwenye sehemu ya wazazi (mobile money: Airtel, Tigo/Yas, Halotel, M-Pesa kupitia ClickPesa). Akishalipa, matokeo yanafunguka mara moja na kubaki wazi mwaka mzima. Shule hailipi chochote. Sharti: angalau asilimia 70 ya wanafunzi wawe wamelipa ndani ya miezi 6 tangu usajili, la sivyo shule inaombwa kuhamia Njia B. Fuatilia maendeleo kupitia Admin Settings › Contribution Settings (waliolipa, wanaotarajiwa, kilichokusanywa, hali ya hatari).

Njia B — shule inalipa ada ya mfumo

Weka Admin Settings › Contribution Settings kuwa School. Kisha Admin Settings › Make Payment: chagua kipindi (TERM au ANNUAL), uone kiasi + VAT, ukalipe kwa M-Pesa Lipa Namba 4350411 (jina: ONESTORE TECHNOLOGIES COMPANY LIMITED): piga *150*00# → 4 Lipa kwa M-Pesa → 1 Weka Lipa Namba → 4350411 → kiasi → PIN. Kisha ingiza Transaction ID kutoka kwenye ujumbe wa M-Pesa chini ya Confirm Payments; uthibitisho unakuja kwa SMS ndani ya dakika chache. Chapisha risiti kupitia Admin Settings › Print Receipts.

Ada ya mfumo ikichelewa, kwanza unaona “Warning: System Fee Awaiting Payment” (baadhi ya huduma zinasimama), kisha “Service Suspended”. Ukilipa, akaunti inafunguka yenyewe.

Huduma nyingine za kulipia: vifurushi vya SMS (TZS 35 kwa SMS) na namba yako mwenyewe ya WhatsApp (TZS 10,000/mwezi). WhatsApp kutoka namba ya pamoja ya FAMNET ni bure.

Hukupata jibu? Andika WhatsApp kwa msaada wa FAMNET: 0722 279 412 (ujumbe tu), piga simu 0753 464 603 (simu tu), au barua pepe [email protected].