Ruka hadi maudhui

Masomo: kusajili, kuyapangia madarasa, masomo-ndani na combinations

Sajili kila somo mara moja, lipangie ngazi za madarasa yanayolisoma, na (ukipenda) ugawe somo kwenye masomo-ndani yenye asilimia.

Imesasishwa 06/10/2026

Admin Settings › Subjects Registration

1. Sajili masomo

Ingiza Subject Name (mf. Mathematics), Subject Type (Core / Optional), Subject Report Name (jinsi linavyochapishwa kwenye ripoti, mf. “MATHEMATICS”) na Subject Short Name (mf. MATH, hutumika kwenye majedwali membamba) → Submit. Bofya jina lolote kwenye jedwali la mwonekano ili kulihariri.

2. Panga masomo kwa ngazi za madarasa

Ama chagua ngazi moja ya darasa ukatiki masomo yake, ama tumia Bulk Assign: tiki masomo mengi na madarasa mengi, kisha Assign selected subjects to selected classes. Kwenye mwonekano, bofya darasa chini ya “Class Assigned” ili kuondoa mpangilio huo.

Somo linaonekana kwenye Excel ya matokeo ya darasa pale tu limepangiwa ngazi hiyo. Mwalimu akisema “somo langu halipo kwenye karatasi ya kupakia”, hapa ndipo pa kurekebisha.

3. Masomo-ndani (si lazima)

Admin Settings › Assign Sub Subjects: chagua darasa na Main subject (mf. Science), tiki masomo-ndani (Physics, Chemistry, Biology) ukaweke contribution type — Percent each (mf. 33.3%) au wastani. Walimu wanapakia masomo-ndani; somo kuu linahesabiwa na mfumo.

4. Combinations za A-Level na programu za chuo

Admin Settings › A-Level Combinations — sajili PCM, PCB, HGL, EGM… Wanafunzi wanaunganishwa na combination wakati wa usajili. Vyuo vinasajili Programs (namba, jina, jina fupi, kategoria, ngazi) kupitia Admin Settings › Programs.

Hukupata jibu? Andika WhatsApp kwa msaada wa FAMNET: 0722 279 412 (ujumbe tu), piga simu 0753 464 603 (simu tu), au barua pepe [email protected].