Ruka hadi maudhui

Matatizo ya matokeo: somo halipo, nafasi si sahihi, wazazi hawaoni matokeo

Ufumbuzi wa haraka wa maswali ya kawaida ya matokeo.

Imesasishwa 06/10/2026
DaliliSababu → ufumbuzi
Somo halipo kwenye Excel ya kupakiaHalijapangiwa ngazi hiyo (Admin Settings › Subjects Registration) au halijapangiwa mwalimu (Staffs › Subjects Teachers).
Mwanafunzi hayupo kwenye ExcelHajasajiliwa kwenye darasa/mkondo huo, au amefukuzwa. Msajili/mrejeshe, kisha pakua Excel tena.
Wastani au nafasi inaonekana si sahihiSomo bado halijapakiwa (angalia Marks Completeness), mtihani wa mwisho umepakiwa kama mwezi, au mipaka ya gredi imebadilishwa → Recalculate.
Divisheni inaonyesha “-” au 0 kwa woteDivisheni/pointi hazijawekwa kwa ngazi hiyo, au Results Calculation ipo kwenye Average.
Wazazi wanaona “hakuna matokeo”Muhula haujachapishwa (publish), au mchango haujalipwa.
Mwalimu hawezi kupakia (“locked”)Matokeo yamechapishwa — ofisi ya taaluma i-unpublish kwanza.
Ripoti inachapishwa bila nembo/kichwa/maoniGeneral Settings (nembo, kichwa), Evaluation na Report instructions hazijajazwa.
Ukurasa unaonyesha hitilafu (500)Pakia upya mara moja; ikiendelea, tuma anwani ya ukurasa na muda kwa msaada — mara nyingi ni darasa lisilo na wanafunzi au alama bado.

Hukupata jibu? Andika WhatsApp kwa msaada wa FAMNET: 0722 279 412 (ujumbe tu), piga simu 0753 464 603 (simu tu), au barua pepe [email protected].