Ruka hadi maudhui

Kusajili shule yako

Fungua akaunti ya shule kutoka kwenye tovuti ndani ya dakika tano. Unahitaji jina la msimamizi, jina la shule, aina, simu, barua pepe na nenosiri.

Imesasishwa 06/10/2026
  1. Fungua schools.famnet.co.tz ukabofye Register (au Login → Register your school).
  2. Jaza fomu: Full Name of Admin (jina la msimamizi), School Name, School Type (Primary / Secondary / College), School Ownership (Serikali / Binafsi), School Reg Number (namba ya kituo, mf. S1234 au PS0101234 — si lazima ila inashauriwa), School Email, School Mobile (tiki “This number is on WhatsApp” ili upokee matokeo, ada na matangazo bure), anwani, eneo, nchi, tovuti, Login Header Message (ujumbe unaoonekana kwenye ukurasa wa kuingia, mf. “Karibu Hope Secondary School”) na Password.
  3. Kubali masharti ukabofye Register School.
  4. Ingia kwa School Reg Number (au barua pepe kama hukutoa namba ya usajili) na nenosiri lako.
Ujumbe “It seems this school is already registered” unamaanisha kuna shule yenye namba hiyo au barua pepe hiyo tayari. Tumia Login au Forgot password, au wasiliana na msaada ili akaunti ikabidhiwe kwako.

Ukishasajili, nenda moja kwa moja kwenye orodha ya mipangilio ya kuanzia — matokeo na ripoti hutoka sawa tu pale madarasa, masomo, gredi na ada zimepangwa.

Hukupata jibu? Andika WhatsApp kwa msaada wa FAMNET: 0722 279 412 (ujumbe tu), piga simu 0753 464 603 (simu tu), au barua pepe [email protected].