Results/Matokeo inaonyesha matokeo yaliyochapishwa ya kila muhula: alama za kila somo, gredi, wastani/pointi, divisheni, nafasi, maoni ya mwalimu wa darasa na mahudhurio — yanachapishwa.
Mchango wa mfumo
Kama shule yako inaruhusu wazazi kulipa mmoja mmoja, mara ya kwanza unapofungua matokeo unaona “Matokeo yapo tayari — kamilisha mchango wa mfumo”. Ni TZS 3,500 kwa mwaka mzima, unalipwa mara moja:
- Ingiza namba ya simu itakayolipa ukachague mtandao (Airtel, Tigo/Yas, Halotel, M-Pesa).
- Bofya LIPA SASA; ujumbe wa USSD unatokea simuni — weka PIN yako.
- Matokeo yanafunguka mara moja. Historia ya Malipo inaonyesha malipo yako na namba za kumbukumbu.
Shule zinazolipa ada ya mfumo zenyewe zinaonyesha matokeo bila hatua hii.