Ruka hadi maudhui

Malipo ya ada mtandaoni ya wazazi — mhasibu anaona nini

Wazazi wanalipa kutoka simuni; malipo yanaingia yenyewe kwenye vitabu vya malipo na risiti ya shule. Hakuna cha kuingiza tena — hakiki tu na uendelee.

Imesasishwa 06/10/2026

Wazazi wanalipa kwenye ukurasa wa Lipa Ada wa sehemu ya wazazi kwa njia tatu: USSD push kwenye simu (Airtel/Tigo/Halotel), namba ya malipo (control number) inayolipwa kwa M-Pesa, Airtel Money, Mixx by Yas, Halopesa na CRDB/benki, au (ikiwashwa) ukurasa wa benki/kadi. Wazazi wanavyolipa.

Kinachotokea malipo yakikamilika

  • Yanarekodiwa kama uingizaji wa mhasibu: benki ClickPesa (Mobile Money), issuer PARENT-ONLINE, njia Mobile Money au Bank, na risiti ya shule (R…). Yanaonekana kwenye kila ripoti ya malipo na salio la mwanafunzi linapungua mara moja.
  • Mzazi anapata risiti ya Kiswahili kwa WhatsApp/SMS; wafanyakazi wa fedha na namba ya shule wanapata taarifa ya Kiingereza.

Ukurasa wa mhasibu

Payments › Online Fee Payments (ClickPesa): kila jaribio na tarehe, mwanafunzi, darasa, ada, kiasi, simu, njia (USSD push / Control No. / Checkout link na mtandao au benki iliyolipa), hali (COMPLETED, PENDING, FAILED), risiti ya shule na kumbukumbu ya ClickPesa. Vigae vinaonyesha kilichokusanywa mtandaoni, idadi ya yaliyokamilika na yanayosubiri. Tumia kumbukumbu ya ClickPesa kulinganisha na settlement kwenye dashibodi yako ya ClickPesa.

PENDING yenye namba ya malipo inamaanisha mzazi ana namba ila bado hajalipa — haina muda wa kuisha. USSD push zilizo FAILED ni jambo la kawaida (mzazi alighairi au hakuwa na salio).

Hukupata jibu? Andika WhatsApp kwa msaada wa FAMNET: 0722 279 412 (ujumbe tu), piga simu 0753 464 603 (simu tu), au barua pepe [email protected].