Ruka hadi maudhui

Kupanga muundo wa ada (aina za malipo, viwango, awamu, vipaumbele, benki)

Mipangilio mitano, inayofanywa mara moja kila mwaka wa masomo, inayowezesha kuingiza malipo, salio, SMS za madeni na malipo ya ada mtandaoni.

Imesasishwa 06/10/2026

Yote yapo chini ya Admin Settings (shule za sekondari zina kurasa tofauti za O-Level na A-Level). Fanya kwa mpangilio huu:

1. Payment Types

Sajili kila aina ya malipo: School Fee, Food Fee, Transport, Uniform, Initial costs, Examination… Kisha assign students on payments required: tiki ngazi za madarasa na aina ya mwanafunzi (Day only / Boarding only / Day and Boarding) wanaotakiwa kulipa kila aina. Bofya jina la aina ya malipo ili kuifanya default (inachaguliwa yenyewe wakati wa kuingiza malipo na ndiyo ya kwanza mzazi anayolipa mtandaoni).

2. Fee Amounts

Kwa mwaka wa masomo unaoonekana (ubadilishe kwa Change academic Year), ingiza Total Amount (TSh) kwa kila aina ya malipo × ngazi ya darasa × aina ya mwanafunzi. Hiki ndicho kiasi mwanafunzi anachotarajiwa kulipa kwa mwaka.

3. Set Installments

Idadi ya awamu na kiasi cha kila awamu (mf. awamu 3 za 400,000). Hutumika kwa “Installments alert” na vikumbusho vya malipo.

4. Payments Priorities

Mpangilio wa kugawa fedha mzazi akilipa bila kutaja aina (1 = ya kwanza). Pia hutumika kwa priority alert.

5. Bank Accounts

Sajili akaunti/njia ambazo malipo yanaingia: jina la benki na jina la akaunti (CRDB — Hope Sec, NMB, Cash, M-Pesa). Kila malipo yanayoingizwa yanawekewa moja, na hivyo ripoti ya Payments by bank inawezekana. Mfumo unaongeza ClickPesa (Mobile Money) wenyewe kwa malipo ya mtandaoni.

Punguzo la mwanafunzi mmoja (ufadhili, watoto wa walimu) linawekwa kwenye wasifu wa mwanafunzi kupitia Students › Students List kama kiasi kilichopunguzwa; salio na ukurasa wa Lipa Ada wa mzazi vinatumia kiasi hicho kilichopunguzwa.

Hukupata jibu? Andika WhatsApp kwa msaada wa FAMNET: 0722 279 412 (ujumbe tu), piga simu 0753 464 603 (simu tu), au barua pepe [email protected].