Ruka hadi maudhui

Mtiririko wa matokeo: kutoka alama hadi ripoti zilizochapishwa

Hatua sita za kila muhula — mipangilio, kupakia, kukagua ukamilifu, kuona/kuhesabu upya, kutathmini, kuchapisha na kutuma.

Imesasishwa 06/10/2026
  1. Mipangilio iko tayari — masomo yamepangiwa madarasa, aina ya tathmini, gredi, divisheni/pointi na njia ya hesabu (Admin Settings). Walimu wamepangiwa masomo na madarasa.
  2. Walimu wanapakia alama — kwa kila somo, kila darasa, kila mwezi (CA) au kila muhula (mtihani wa mwisho/wa mwaka). Kupakia matokeo
  3. Ukamilifu wa alama — ofisi ya taaluma inakagua darasa/muhula/mwezi gani bado unakosa masomo. Ukamilifu wa alama
  4. Kuona na kuhesabu upya — angalia matokeo ya darasa, wastani, gredi, divisheni na nafasi; hesabu upya baada ya marekebisho yoyote. Kuona matokeo
  5. Tathmini na maelekezo ya ripoti — walimu wa madarasa wanaongeza maoni na ujumbe wa muhula. Kutathmini wanafunzi
  6. Kuchapisha (Publish) — inafunga alama, inafungua matokeo kwa wazazi mtandaoni na kuwezesha SMS/WhatsApp za matokeo; kisha chapisha ripoti za wanafunzi na karatasi za darasa. Kuchapisha matokeo
Mihula: Term I ≈ Januari–Juni, Term II ≈ Julai–Desemba (menyu ya Term II inaonekana kuanzia Julai). Alama za kila mwezi/katikati ya muhula ni CA; mtihani wa mwisho ni matokeo ya muhula; matokeo ya Annual yanaunganisha mihula yote miwili.

Hukupata jibu? Andika WhatsApp kwa msaada wa FAMNET: 0722 279 412 (ujumbe tu), piga simu 0753 464 603 (simu tu), au barua pepe [email protected].