Students › Register Students (ukurasa wa O-Level, A-Level, Primary, Nursery au College kulingana na aina ya shule yako).
A. Mwanafunzi mmoja au wachache — fomu
Jaza: Full Name, Gender, Birthday, Admission Year, Scholar Type (Day / Boarding), Class Admitted, Stream, Admitted From (shule aliyotoka), Admission Number (namba yenu wenyewe, si lazima), Place of Residence, Nationality, Email, Parent's Mobile Number (inatumika kwa SMS/WhatsApp na kama mawasiliano ya mzazi — iandike kama 07XXXXXXXX). Msingi ina pia PREM Number na Exam Number; A-Level ina Combination. Bofya Submit.
B. Darasa zima — Excel
- Chini ya Register Students By Excel Here chagua ngazi ya darasa ukapakue kiolezo.
- Jaza mwanafunzi mmoja kwa kila mstari, ukizingatia mpangilio na vichwa vya safu kama vilivyo; usiunganishe seli wala kuongeza sheet nyingine. Jinsia M/F, tarehe DD/MM/YYYY, aina ya mwanafunzi Day au Boarding.
- Chagua ngazi ya darasa, chagua faili ukabofye Submit. Utapata Upload Summary (imehifadhiwa) au orodha ya makosa: FILE FORMAT ERROR = kiolezo/format si sahihi (hifadhi kama .xlsx kutoka kwenye kiolezo); Students with no scholar type = safu ya Scholar Type ni tupu kwa mistari hiyo — hakuna kinachohifadhiwa hadi urekebishe na kupakia tena.
Namba za usajili
Mfumo unatengeneza namba ya usajili wenyewe: kiambishi cha ngazi + namba ya shule + mwaka wa kujiunga + namba ya mfululizo, mf. OS121.2025.015 (O-Level, shule S.121, aliyejiunga 2025, wa 15). Wazazi wanaingia kwa namba hii; inachapishwa kwenye ripoti na risiti na haibadiliki hata mwanafunzi akipanda darasa.