Ruka hadi maudhui

Wazazi: jinsi ya kuingia

Jina la mtumiaji = namba ya usajili ya mwanafunzi; nenosiri = jina la mwanafunzi kama lilivyosajiliwa shuleni.

Imesasishwa 06/10/2026
  1. Fungua schools.famnet.co.tz → Login (au bofya Ingia kama mzazi).
  2. Jina la mtumiaji: namba ya usajili ya mwanafunzi iliyochapishwa kwenye ripoti / risiti au uliyotumiwa kwa SMS/WhatsApp, mf. PS122.2026.534.
  3. Nenosiri: jina kamili la mwanafunzi kama shule ilivyomsajili (sehemu ya jina kwa kawaida inatosha, mf. jina la kwanza na la mwisho).

Unafika kwenye sehemu ya wazazi: Student/Mwanafunzi (wasifu), Results/Matokeo, Payments/Malipo, Lipa Ada/Pay Fees, News/Habari.

Umeshindwa kuingia? Uliza ofisi ya shule namba sahihi ya usajili na jinsi jina lilivyoandikwa. Kila mtoto ana akaunti yake.

Hukupata jibu? Andika WhatsApp kwa msaada wa FAMNET: 0722 279 412 (ujumbe tu), piga simu 0753 464 603 (simu tu), au barua pepe [email protected].