- Msimamizi wa shule — kwenye ukurasa wa kuingia bofya Forgot password, ingiza namba ya usajili/barua pepe ya shule; msimbo wa kurejesha unatumwa kwa barua pepe/WhatsApp ya shule. Kama huna tena barua pepe au namba hiyo, andika WhatsApp kwa msaada 0722 279 412 (au piga simu 0753 464 603) ukitaja jina la shule na namba ya usajili.
- Walimu — mwombe msimamizi wa shule: Human Resource › Employee List › Password restore inarudisha nenosiri kuwa default; ingia ukalibadilishe.
- Wazazi — hakuna nenosiri la kurejesha: jina la mtumiaji ni namba ya usajili, nenosiri ni jina la mwanafunzi kama lilivyosajiliwa. Hakikisha vyote na ofisi ya shule.
Nenosiri lililosahaulika
Msimamizi wa shule: tumia Forgot password kwenye ukurasa wa kuingia. Walimu: msimamizi analirudisha kuwa “default”. Wazazi: nenosiri ni jina la mwanafunzi.
Imesasishwa 06/10/2026
Hukupata jibu? Andika WhatsApp kwa msaada wa FAMNET: 0722 279 412 (ujumbe tu), piga simu 0753 464 603 (simu tu), au barua pepe [email protected].