Ruka hadi maudhui

Kutathmini wanafunzi (maoni ya mwalimu wa darasa)

Kila muhula mwalimu wa darasa anampa kila mwanafunzi gredi kwenye vigezo vya tathmini na kuandika maoni; yanachapishwa kwenye ripoti.

Imesasishwa 06/10/2026

Evaluation › Evaluate Students → Term I / Term II → darasa lako (wafanyakazi wa taaluma wanaona All classes). Ukiona “No any class assigned to you”, mwombe msimamizi akufanye mwalimu wa darasa (Staffs › Class Teachers).

  1. Orodha ya darasa inafunguka na safu moja kwa kila kigezo kilichowekwa kwenye mipangilio ya tathmini (Conduct, Discipline, Punctuality…). Chagua gredi (A–D) kwa kila mwanafunzi, ongeza maoni ya mwalimu wa darasa na, pale ilipowashwa, maoni ya mkuu wa shule.
  2. Submit. Unaweza kurudi na kuhariri hadi matokeo yachapishwe.

Evaluation › View Evaluations inaorodhesha yaliyoingizwa kwa kila darasa. Maoni yanachapishwa kwenye ripoti ya mwanafunzi chini ya matokeo ya masomo.

Hukupata jibu? Andika WhatsApp kwa msaada wa FAMNET: 0722 279 412 (ujumbe tu), piga simu 0753 464 603 (simu tu), au barua pepe [email protected].